Friday, July 18, 2014

UGANDA KUANZA KUTENGENEZA MAGARI

Uganda itaanza utengenezaji wa magari mwaka wa 2018, imetangaza serikali ya Uganda. Profesa Sandy Stevens, ambaye ni afisa mkuu wa mradi unaopanga kuanzisha uundaji wa magari hayo, anasema ifikap mwaka huo kila kitu kitakuwa tayari kuanza kazi hiyo.

Mhandisi mkuu wa mradi huo Isaac Musasizi anasema watahitaji dola za kimarekani milioni 350, kupanga kila kitu pamoja na kujenga kiwanda cha uundaji wa magari hayo. Anasema pia magari yakakayo kuwa yakiundwa na nchi hiyo, ni sawa na lile lililozinduliwa na rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni, mwaka wa 2011.

Waziri wa biashara na viwanda nchini humo Amelia Kyambadde, anasema kuanza kwa mradi huo wa uundaji magari ni moja wapo ya mipango ya serikali yake, ya kuipa nchi hiyo maendeleo ya kiuchumi. Hata hivyo serikali ya Uganda inasema itashirikiana na kampuni moja ya Kimataifa, ili kuhakikisha magari yao yanatambulika kimataifa pindi tu yatakapoanza kuuundwa.



Name:  mobius-2-876.jpg
Views: 0
Size:  79.1 KB

No comments:

Post a Comment