|
kutoka Kushoto ni Rose Simion kutoka Ulemo na Grace ernest kutoka Shelui |
Leo katika kutembelea maonyesho ya wakulima nane nane yanayofanyika kikanda kwa kanda ya kati yanafanyika Dodoma na Kitaifa yanafanyika Mkoani Lindi, nilifanikiwa kukutana na wakinamama wawili mmoja anaitwa Grace ernest kutoka Shelui na Rose Simion kutoka Ulemo wakiwa ni wawakilishi kutoka kwenye vikundi vyao, katika mojawapo ya banda la Wilaya ya iramba wakiwa na bidhaa zitokanazo na mafuta ya alizeti yaliyoongezewa thamani. Katika mnyoro wa thamani wa zao la alieti wamefanikiwa kutengeneza mafuta ya kupaka (mgando), dawa ya mbu (mosquitoe reppelant), Dawa ya ngozi (medicinal oil), Rangi ya viatu pamoja na mkaa utokanao na mabaki ya zao la alizeti.
|
rose mafuta ya dawa |
wanasema wamepata mafunzo hayo kupitia mradi wa PEML (Producer empowerment and Market linkage) kupitia MIVARF wakiwa chini ya usimamizi wa RCCL (Rural Consultancy company Limited) bofya hapa wakiwa watoa huduma (Service Provider) katika eneo lao la mradi. Pia kupitia mtoa Huduma RCCl wamefanikiwa kuunganishwa na masoko ya bidhaa zao, elimu juu ya uzalishaji wa zao la alizeti wenye tija, elimu ya fedha, usindikaji nk.
|
Malaika mafuta ya kupaka |
|
Rose simion akiwa na mafuta ya Alizeti |
No comments:
Post a Comment