Baada ya kukutana na maswali mengi kutoka kwa wadau wa kilimo wakisema wanasumbuliwa na ugonjwa huu pia waweza sema ni disorder katika mazao ya nyanya, pilipili hoho pamoja na tikiti maji. Yafuatayo ni maelezo mafupi ya ugonjwa husika Kidonda cheusi kilichodidimia huonekana kwenye kitako cha tunda. Kisha sehemu hii hunyauka na ngozi huwa nyeusi. Hali hii hutokea zaidi wakati wa jua kali na katika sehemu zenye udongo wenye chumvichumvi na tindikali nyingi. Pia nyanya nyingine huwa na makunyanzi upanda wa chini wa tunda na kuoza. Sehemu hiyo huwa na rangi nyeupe.
VISABABISHI
• Upungufu wa calcium wakati wa ukuaji wa tunda.
• Upungufu wa calcium wakati wa ukuaji wa tunda.
• Kumwagilia pasipo kuwa na mtiririko maalumu
• Kuzidisha matumizi ya mbolea yenye kiambata cha N (Urea)
KUZUIA
• Kuzidisha matumizi ya mbolea yenye kiambata cha N (Urea)
KUZUIA
- Epuka kulima kwenye maeneo yenye hali ya chumvichumvi na tindikali nyingi.
- Usibadilishe nyakati za kumwagilia
- Punguza matumizi ya mbolea yenye kiambata cha N
0 comments:
Post a Comment