Tasnia ya ufugaji wa samaki inajumuisha ukuzaji wa viumbe vya kwenye maji (bahari na maji baridi)
katika mazingira tofauti na yale ya asili. Lengo kuu ni kukuza kwa muda mfupi ili kujipatia lishe,
kipato na kutunza mazingira ya bahari, mito, maziwa nk.
Ufugaji unagusa viumbe vya kwenye maji kuanzia mimea kama vile mwani, samaki wasio na mapezi
(kaa-crabs, kambamiti-prawns, chaza-oyster, majongoo bahari nk) na samaki wenye mapezi
(perege/sato, kambale, kibua, trout, chewa nk).
Aina ya ufugaji
Zifuatazo ni aina/level za ufugaji ambazo mkulima anaweza kufanya kulingana na malengo na uwezo
wake:
1. Huria (Extensive farming)
- Idadi ya samaki wanaopandikizwa: samaki 2-3 kwa mita ya mraba
- Samaki hutegemea chakula cha asili (mimea ya majini-phytoplankton,
- wadudu/viumbe vidogo vya majini-zooplankton) Hauitaji ubadilishaji wa maji
- Hauihitaji huduma ya ziada ya hewa
- Idadi ya samaki, 4-7 kwa mita ya mraba
- Chakula cha asili na chakula cha ziada huitajika
- Maji hubadilishwa sentimenta 10-20 kila baada ya 3-4weeks kulingana na hali ya samaki na maji yako
- Huduma ya hewa ya ziada sio ya ulazima
- Idadi ya samaki kwa mita ya mraba ni 10-25
- Chakula cha asili na cha ziada
- Huduma ya hewa ya ziada lazima
- Maji hubadilishwa kila siku au kila baada ya siku kadhaa (15-25 cm)
- Idadi ya samaki ni zaidi ya 25 kwa mita ya mraba
- 100% chakula cha kutengenezwa
- Maji ni kuingia na kutoka
- Hewa ya ziada masaa yote
- Eneo linalotumika ni dogo ukilinganisha na mifumo mingine
Samaki wanaweza kufugwa katika miundombinu mbalimbali kama ifuatayo:
- Bwawa
- Kina 0.8-1.5m, Ukubwa 100 mita za mraba
Kina 1-1.5m
Kipenyo kwa lile la mduara 3
Ukubwa kwa la mstatili inategemea na uwezo lakini lisiwe kubwa ili kuhimili nguvu ya maji
Materials: Plastic, cement, chuma nk
NB: Simtank linafaa( Faida inapatikana kama utalitumia kwa intensive system)
Vizimba (Fish cages)
Huwekwa katika maji ya asili kama vile ziwani, baharini au katika bwawa. Vipo vinavyoundwa
kwa local materials kama mianzi na vipo vya aluminium
Eneo linalofaa kwa ufugaji
Baadhi ya maeneo yanayofaa ni yale mashamba ya mpunga, na maeneo yaliyo karibu na vyanzo vya
maji. Zifuatazo ni sifa za maeneo yanayofaa:
1. Udongo: Mfinyanzi husaidia kupunguza gharama za ujenzi wa bwawa na maji kwakuwa
linaweza kutuamisha maji na kuruhusu maji yasipotee. Likiwa la kichanga bwawa ni lazima
lijengewe au kuwekwa nylon sheet ili kuzuia upotevu wa maji. Unaweza ukahamisha udongo
wa mfinyanzi kutoka sehemu moja hadi nyingine ili kuzuia upotevu wa maji (muone
mtaalamu kwa ushauri zaidi juu ya mbinu ya kuhamisha udongo)
2. Chanzo cha maji ya uhakika
Eneo liwe na maji ya uhakika. Vyanzo vya maji ni kama vile mito, bahai, maziwa, chem
chem., kisima, maji ya dawasco na mvua. Maji yasiwe na kemikali hatarishi kwa viumbe.
3. Miundombinu ya barabara: Inasaidia kwa ajili ya usafirishaji wa bidhaa na samaki wakati wa
kuvuna.
4. Eneo lisiwe na historia ya mafuriko ili kuzuia athari za mafuriko kwa miundombinu yako.
Utatumia gharama nyingi katika kuimarisha miundombinu yako.Jamii/aina ya samaki
5. Eneo lenye mwinuko wa wastani husaidia katika ujenzi wa bwawa.
6. Miundombinu ya umeme ni sifa ya ziada hususan kwa mkulima wa kati na wajuu kwa ajili ya
kutumika katika kuendesha visambaza hewa.
7. Ulinzi muhimu
Note: Aina ya eneo lako ndilo linaweza kukufanya uchague muundombinu gani wa kufugia
utumie
Aina ya samaki unaoweza kufuga Tanzania kwa sasa
Maji baridi
Sato/perege, Kambale, Kambamiti wa maji baridi na Trout (maeneo ya baridi kama vile
Iringa, Kilimanjaro Arusha na Mbeya) na samaki wa mapambo.
Maji bahari
Kambamiti wa maji bahari, mwatiko, chewa, kaa, chaza wa lulu
Upatikanaji wa Vifaranga vya samaki husika
Vyanzo vya vifaranga ni kutoka katika mito, bahari, maziwa na wale wa kuzalishwa katika
vituo vya kuzalishia vifaranga.
Sato na Kambale
Vituo vya serikali Utapata sato wa kike na kiume mixed sex). Kingolwira –Morogoro, Luhira-
Songea, Mbegani-Bagamoyo . Kifaranga huuzwa Tsh. 50-100 kwa kifaranga.
Vituo binafsi kama vile Faith aquaculture-Kibamba (DSM) (utapata monosex sato), Peramiho-
Songea (mixed sex). Monosex huuzwa Tsh. 200 kwa kifaranga, na mixed ni 100 kwa kifaranga.
Chakula cha samaki
Chakula cha asili
Hurutubishwa kwa mbolea ya wanyama kama vile kuku, ngombe, mbuzi nk. Kwa kiwango
cha 1000kg/ha. Mbolea ya kuku ni kali hivyo unaweza punguza ikawa 250-500kg/ha.
Chakula cha kutengeneza
Samaki huitaji protein ili akuwe na kila samaki ana mahitaji yake hivyo ni species specific.
Formula zipo kwa wale wanaotaka kutengeneza. Tanzania hakuna kiwanda
kinachotengeneza. Ingredients zake ni kama vile dagaa, pumba, soya, unga wa ngano, unga
wa muhongo nk.
Uvunaji
Kwa kawaida ni miezi 4-6 amabapo unapata 250-400g kulingana na ulishaji wako. Kwa
prawns ni miezi 3-6 wanafikia 30-50g ambayo ni ukubwa wa soko.
Tathmini ya uchumi
Perege/sato
Mfano:
Ukubwa wa bwawa ni 20m by 30m= 600 mita za mraba
Idadi ya samaki (7 kwa mita ya mraba) kwa monosex tu= 600 x 7=4200 fish
Uzito hadi kuvuna (4-6months)- 250g= 4200 x 250g= 1050kg (Nimesha convert gram to kg)
Bei kwa kilo ni 6000-8000 kulingana na mahali= 6milion-8milion.
Gharama unazoweza kutumia
Ujenzi wa bwawa
Kuchimba kwa vibarua ni 500,000-600,000
Kuchimba kwa machine ni 1,000,000-1,500,000 kulinganana mahali ulipo
Kama udongo ni kichanga itabidi ujengee (kujengea ni gharama na inaweza ikafika 3.5-4m
kwa gharama zote kuanzia kuchimba hadi kujengea).
Chakula cha kutengeneza tani 1 inaweza kugharimu laki 7-9. Hapa ili uweze kuzalisha tani 1
ya samaki aina ya perege utahitaji tani 1-1.5 ya chakula.
Gharama ya vibarua 150,000-250,000 kwa mwezi.
Utakuwa na gharama ya chokaa kwa ajili ya kuua vidudu (laki 100,000-200,000), mbolea
kuzalisha chakula cha asili (gharama ni 50,000).
No comments:
Post a Comment