AINA ZA NGURUWE




1.    Utangulizi

·         Nguruwe ni jamii ya wanyama wasiocheua, na wenye kwato zilizogawanyika.
·         Wanyama wengine walio kwenye jamii hii ni pamoja na Nguruwe pori na Ngiri
·         Nguruwe wanafugwa maeneo mengi duniani kwa zaidi ya miaka elfu moja iliyopita
·         Nguruwe ni kati ya mifugo iliyoonyesha ufanisi mkubwa wa kutoa nyama na fedha kwa kipindi cha muda mfupi na hivyo kufanya kuwa aina ya mfugo anayapependwa kwenye nchi mbalimbali kwa ajili hasa ya nyama na fedha

2.    Faida za ufugaji wa nguruwe

·         Nguruwe ni mnyama anayekuwa kwa haraka sana kuliko baadhi ya mifugo mingine kama: Ng’ombe, Mbuzi na Kondoo
·         Nguruwe huzaa na kuongezeka kwa wingi
·         Anauwezo wa kutumia mabaki yasiyowezekana kwa matumizi mengine
·         Anauwezo wa kutoa mafuta kwa ajili ya kupika
·         Anauwezo wa kutengeneza fedha za haraka kwa ajili ya uwezo wake wa kuzaa kwa haraka na watoto wengi
·         Ni rahisi kuwalisha nguruwe
·         Wanaweza kukuzwa kwenye eneo dogo
·         Nyama yake ni laini na yenye viini lishe vingi
·         Huzalisha mbolea iliyobora kwa matumizi ya kilimo


3.  Aina za nguruwe

Humu nchini mwetu kuna kuu tatu za nguruwe
i.       Nguzuwe wa kienyeji
ii.     Nguruwe weye asili ya ugenini (Exotic breed)
iii.    Nguruwe mchanganyiko (crosses): wenye mchanganyiko wa damu ya kienyeji na ugenini ( Local x Exotic) na wenye mchanganyiko wa damu za ugenini (exotic x exotic) 



Aina za Nguruwe (breeds) wenye asili ya ujenini zinazopatikana kwa wingi kwenye mazingira yetu.

i.     Large white

Sifa
·         Rangi nyeupe
·         Miili mikubwa
·         Masikio yaliyosimama wima
·         Wana asili ya Uingereza
·         Wanauwezo wa kuzaa watoto wengi
·         Wana nyama nzuri
·         Wana uwezo mzuri wa ukuaji



ii.   Landrace

Sifa
·         Rangi nyeupe
·         Miili huwa na umbo refu na huonekena wembamba
·         Masikio yaliyolala na kufunika sehemu ya macho
·         Wanaasili ya Denmark
·         Ni wazazi wazuri
·         Ni wazuri kwa nyama
                                                    


 iii.  Saddle back
Sifa
·         Mwili wenye rangi  nyeusi ulio na mshipi mweupe unaopitia kwenye mabega
·         Masikio ya kulala
·         Wana asili ya Uingereza



NB.    Aina zi za nguruwe zilizotajwa hapa juu wengi wao wamekaa Kwa muda mrefu hivyo kupoteza nasaba yake kutokana na muingiliano wa vizazi mablimbali
Share on Google Plus

About kilimo uchumi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment