UTANGULIZI
Ni ugonjwa (Kuhara kinyesi cheupe) unao enezwa na bacteria (salmonella pullorum) Mzunguuko wa maambukizi ya ugonjwa huu hupitia kwenye mayai ya kutotorewa hadi kwa Vifaranga. Vifaranga huambukizwa kirahisi mnamo wiki 3 za mwanzo kwa kula chakula chenye bakteri wa ugonjwa huu.
Dalili za ugonjwa kwa Vifaranga:
- Vifo vingi kutokea kwenye siku 10 za mwanzo
- Kutokuwa na hamu ya kula
- Vifaranga kuzubaa
- Kulegea kwa mabawa na manyoya kuchachamaa
- Kuvimba matumbo
- Vifaranga kupiga kelele na kuzubaa huku wamefumba macho
- Kuharisha kinyesi cheupe /kinyesi kuganda kwenye sehemu ya kutolea haja
- Vifaranga kuchechemea na kuanguka kabla ya kufa
1.Maini na mapafu kuvimba
2.Mapafu kupauka
3.Maini kuwa meusi mno
4. Moyo kuwa Si wakaida na kuwa na maji maji ya damu
5. Viungo vya miguu na vidole kuvimba.
Dalili za ugonjwa kwa kuku.
- Vilemba au upanga kusinyaaa
- Vifo kutokea Kati ya siku 4 au 5
- Manyoya kuchachamaa
- Kuku kutoa uharo mweupe /unao nuka
- Uzalishaji wa mayai kuwa chini sana.
1. Mayai kwenye sehemu ya kizazi kuwa na rangi ya kijani
kibichi /hadi weusi
2. Mfuko wa kizazi kujaa kiini cha njano cha mayai
3. Ini kuvimba.
4. Uvimbe mdogo mdogo wa kijivu ulioenea kwenye misuri
ya moyo
MATIBABU:
Tumia dawa yenye uwezo wa kuuwa bacteria kama Flume
- Ebs3
- Tremazine 30% Nk.
0 comments:
Post a Comment