MAGONJWA YA VITUNGUU




MAELEZO YA MSINGI KUHUSU MAGONJWA YA VITUNGUU
1. Anthracnose.

kitunguu chenye anthracnose

Ugonjwa huu hutokea shambani muda mfupi kabla ya kuvuna na huendelea mpakawakati wa kuhifadhi. Kama maji yametuama na kuna hali ya joto bustanini, ugojwa huu hujijenga vizuri na husababisha kukauka kwa miche (damping off). Ugojwa huu husababishwa na vimelea vidogo viitwavyo fangasi. Vimelea hivi huishi kwenye vitunguu vilivyoshambuliwa na kwenye udongo.
Dalili za ugonjwa.
Mistari ya kijani iliyokolea au vidoti vyueusi kwenye maganda ya nje ya kitunguu. Vidoti hivi huendelea na kuwa vikubwa na huweza kushambulia kitunguu kizima. Vitunguu vyeupe kama TEXAS GRANO hushambuliwa zaidi kuliko vitunguu vyekundu kama BOMBAY RED na RED CREOLE
NINI CHA KUFANYA
  •  Kuzalishavitunguu vyekundu ambavyo huweza kustahimili ugonjwa huu.
  •  Kuvuna vitunguu vyote mara vinapokomaa.
  •  Epuka vitunguu kupata mvua ama maji kabla ya kuvuna na wakati wa kuhifadhi.
2.MUOZO WA BAKTERIA (Bacterial soft rot)
Image result for bacterial spot in onion

muozo wa Bakteria kwenye kitunguu

Hili ni tatizo kubwa sana wakati wa kuhifadhi vitunguu, bacteria huingia kwenye kitunguu kupitia kwenye shingo ya kitunguu na kufanya sehemu hiyo iwe kama imelowekwa kwenye maji na kuwa laini sana kutokana na kuoza. Pia ugonjwa huu huingia sehemu iliyo na kidonda ama iliyotafunwa na wadudu.Ugonjwa huu huathiri mazao mengine kama karoti, viazi, seleri na mengine.

NINI CHA KUFANYA
  •  Kuacha vitunguu vikomae vizuri kabla ya kuvuna.
  •  Uangalifu mkubwa utumike ili kuepuka kuvikwaruza vitunguu wakati wa kuvuna na kupaki.
  •  Sehemu ya kuhifadhia iwe na hewa ya kutosha ili kuepuka unyevunyevu kenye vitunguu.
  •  Kama vitunguu ni kwa matumizi ya nyumbani vinaweza kuhifadhwa kwenye friji.
Image result for purple blotch in onion

Ugonjwa wa purple Bloch

3.UGONJWA WA MADOA ZAMBARAO (Purple blotch) 
Ugonjwa huu huanza kama vidoa vidogo kwenye majani ambavyo hukua na kuwa na rangi ya zambarao ha kipindi cha unyevunyevu. Baada ya wiki 3-4 majani hugeuka njano na kuanguka.

NINI CHA KUFANYA
  • Kuapanda aina za vitunguu zenye majani yenye nta ambazo hustahimili huu ugonjwa.
  •  Kulima shamba kila baada ya msimu wa vitunguu.
  •  Kuwe na nafasi ya kutosha kutoka mche hadi mche.
  •  Kuondoa mabaki ya mazao shambani.
  •  Kufanya mzunguko wa mazao.
  •  Kuepuka kuzalisha vitunguu kwenye udongo unaotuamisha maji.
KWA UJUMLA ZINGATIA YAFUATAYO
  •  Usiumize vitunguu wakati wa kuvuna ama kupakia.
  •  Usitumie mbolea ya wanyama waliopewa majani ya vitunguu vyene magonjwa.
  •  Usiruhusu maji kutuama shambani kwa muda mrefu.
  •  Epuka kupanda bila kuzingatia nafasi
  •  Tumia aina za mbegu zinazostahimili magonjwa.
  •  Usipande vitunguu mfulullizo sehemu moja, fanya mzunguko wa mazao.
  •  Hifadhi vitunguu sehemu kavu na yenye hewa ya kutosha.
WADUDU WANAOSHAMBULIA VITUNGUU
1. VITHIRIPI VYA VITUNGUU. (Onion thrips)
Wadudu hawa ndio hatari sana na hushambulia vitunguu Afrika nzima. Vithiripi hushambulia mazao mengine mengi yenye majani mapana. Huwa na urefu wa mm 1, laini na hurukaruka sana. Vitunguu vilivyoshambuliwa huonekana na mabaka meupe na mengine huwa na rangi ya almasi upande wa juu wa majani.
Wadudu hawa husababisha vitunguu kushindwa kuzaa vizuri kama wakishambulia wakati vinaanza kutoa balbu.

NINI CHA KUFANYA
1. Hakikisha vitunguu vinapata maji ya kutosha kwani wadudu hawa hushambulia vitunguu visivyomwagiliwa hasa wakati vinaanza kutengeneza balbu.
2.Ondoa magugu yote shambani/bustanini.
3. Ondoa mimea yote iliyoshambuliwa shambani/bustanini.
4. Nyunyuzia dawa za asili kama vitunguu saumu
5. Tumia dawa iitwayo SPINOSAD, ila isitumike ndani ya siku 20-30 kabla ya kuvuna.

KUMBUKA
Dawa za mwarobaini ni nzuri ila zinaweza kusababisha sumu kwenye vitunguu.

2.NZI WA VITUNGUU (Onion fly)
Funza wa nzi wa vitunguu ni hatari sana kwa vitunguu. Wana rangi ya maziwa na hula mizizi, majani hunyauka na kuwa na rangi ya bluu. Mwisho vitunguu huweza kufa. Pia funza hawa huweza kula miche mchanga na kuiuwa kabisa. Pia hupatikana ndani ya balbu za vitunguu. Madhara ya funza hawa ni makubwa sana kwani vitunguu vilivyoshambuliwa nao ni rahisi kupata magojwa mengi. Huwa wengi kipindi cha unyevunyevu. Wadudu watoao funza hawa hawana uharibifu kwa vitunguu. Wadudu hawa wakitokea shambani husababisha kuwepo na nafasi kubwa isiyo na mimea na kumpa mkulima hasara kubwa.

NINI CHA KUFANYA
  •  Epuka kupanda vitunguu kwenye udongo wenye matamahuluku yasiooza vizuri, mfano udongo uliovunwa nyasi ama uliokuwa na magugu mengi sana. Hakikisha mabaki yote ya mimea shambani yameoza vizuri.
  •  Kwenye udongo uliowekwa samadi, subiri muda wa kutosha kabla ya kupanda.
  •  Epuka kupanda vitunguu mfululizo, fanya mzunguko na mazao mengine.
  •  Ondoa vitunguu vilivyoshambuliwa na viharibu kwa moto.
  •  Tifua udongo ili kuuwa mayai ya nzi huyu kwa jua.  
KUMBUKA
  • Pilipili iliyosagwa kuzunguka mashina ya vitunguu husaidia endapo wadudu si wengi sana.


Share on Google Plus

About kilimo uchumi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment