SIRI YA UTAJIRI
JIBU LA KWA NINI WATU WENGINE NI MASIKINI NA WENGINE NI MATAJIRI
Watu wengi wanajiuliza, “Siri ya utajiri ni nini?” Jee ni mbinu gani
zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni kujifunza elimu
ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa
na ziada na faida. Kwa bahati mbaya sana, elimu hii haifundishwi darasani ila
wanayo wafanyabiashara wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri
na huendelea kuificha. Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua
siri ya utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate
manufaa kwa kununua kitabu hiki nimeamua kuiweka siri hii wazi:-
- Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani unaoweza kuitoa ziada na faida.
- Siri ya pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na kujenga tabia ya kuweka akiba
- Siri ya tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega uchumi ambavyo vinazalisha faida endelevu.
- Siri ya nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na kuanzisha biashara yako ili iwe indelevu.
Kuna njia mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika. Njia ya kwanza ni njia ndefu ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya fedha wameigundua njia hii ni rahisi kuifuata kwa sababu haihitaji uwe na kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge tabia ya kuweka akiba, anza kuweka akiba ya T.shs 1,000 kila siku sawasawa na TShs 30,000 kwa mwezi, matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa kipindi cha miaka 65 bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs 23,725,000 (Milioni Ishirini na Tatu Mia Saba Ishirini na Tano Elfu). Kama utawekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa kila mwaka itazaa na kukuletea TShs 2,750,000,000 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Saba Hamsini). Hesabu hii inaweza ikakutisha na usiamini macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu ya hesabu na riba kama alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika dunia hii hakuna kitu chenye nguvu kama hesabu za riba. Pengine njia hii inaweza kuwa ni ndefu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu hatuwezi kusubiri muda mrefu. Hivyo tungependa kuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa haraka. Lakini nasisitiza kama kipato chako ni kidogo anza leo kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.

Dundulizo la akiba hii hukutiririshia utajiri bila wewe kukusudia kwani
utaweza kukidhi hitajiko la ghafla kama kuugua safari ya dharura gharama za
likizo na hata kutumia mbinu hii kama mpango wa elimu kwa watoto wako iwapo
utawaanzishia hivi mara tu kila mmojawapo anapozaliwa au unaweza kuutumia kama
upanga wa siku zijazo kwa mirathi ukianza hivyo leo kwa kupangilia namna hiyo
kwa kila kusudio lako la baadaye.
Hebu tuangalie njia ya pili.
- Njia ya pili ya mkato ni kuongeza kiwango cha kuweka akiba kama wewe ni mtu mwenye shughuli za kuzalisha ziada. Kipato chako kinaweza kuwa kinaongezeka kila mara. Badala ya kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku jiwekee malengo ya kuweka akiba ya TShs 10,000. Anza kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yako hadi utakapofikia lengo la TShs 10,000 au zaidi kwa siku. Badala ya lengo lako kutimia kwa miaka sitini na tano (65) litatimia haraka zaidi. Kwa mfano ukiweka akiba ya TShs 10,000 kwa siku kwa muda wa miaka sita na miezi sita bila riba yoyote utapata TShs. 23,725,000. Ukiwekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa miaka sita na miezi sita utapata TShs. 33,917,505.78. Kama fedha hiyo utaendelea kuweka akiba kwa riba hiyohiyo hadi kufikia muda wa miaka kumi utapata TShs. 63,112,201.43.
Kwa kuwa kitu cha muhimu hapa ni kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo katika kitegauchumi chenye kutoa faida kubwa, utajiuliza jee uwekeze kwenye kitega uchumi chenye kutoa faida kiasi gani? Wataalamu wa mambo ya fedha wanashauri kuwa uwekeze fedha yako kwenye kitegauchumi chenye kutoa faida ya angalau asilimia 10% Kwa mfano unaweza kuwekeza kwenye Akaunti ya TAJIRIKA ya Standard Chatered Bank” inatoa riba ya asilimia kumi 10% pia unaweza kuwekeza kwa kununua hisa katika soko la hisa na mitaji.
Kwa wastani wa watafiti wa masuala ya fedha viwango vya mapato yatokanayo na hisa kwa gawio pamoja na kukua kwa mtaji ni zaidi ya asilimia 11% ambayo ni makubwa kwa kiwango cha kawaida cha asilimia kumi (10%).
Baada ya kueleza siri ya namna ya kupata utajiri nitazitaja njia zingine ambazo zinaweza kukuwezesha kuwa tajiri.
1. Unaweza kurithi mali na fedha kutoka kwa wazazi wako. Hii ni njia ya kubahatisha kwani watu matajiri siyo wengi na hivyo watoto wenye bahati kama hii ni wachache pia.
2. Unaweza kusomea ujuzi au utaalamu katika fani yenye malipo mazuri na kujiajiri mwenyewe. Kwa mfano, unaweza kusomea fani kama ya Uanasheria, Uhasibu na Udaktari au ufundi / sanaa na kadhalika.
3. Unaweza kuanzisha biashara yako na kuiendesha ili kupata ziada kubwa.
4. Unaweza kuendeleza vipaji vyako na kuwa mwanamichezo au msanii wa kulipwa.
5. Unaweza kutunga vitabu juu ya suala lolote unalolijua. Kwa mfano, kama wewe ni mtu uliyebobea katika masuala ya muziki unaweza kutunga kitabu kinachofundisha watu namna ya kuwa mwanamuziki. Watunzi wengi wa vitabu ni matajiri wakubwa. Hii ni kazi unayoweza kuifanya mara moja lakini ukavuna matunda yake kwa muda mrefu sana.
6. Unaweza kuwa mbunifu na kuanza kuuza mawazo yako au kutumia chombo ulichokibuni kukuingizia fedha.
7. Unaweza kucheza bahati nasibu na kushinda. Tatizo hapa soko na wateja wa aina hii ya huduma ni haba. Hiki ni kitu cha kubahatisha na nimekitaja makusudi ili kuwapa onyo wasomaji kwani watu wengi wanapenda sana kucheza michezo ya kubahatisha.
Uwezekano wa kutajirika kwa njia hii ni mdogo sana. Hivyo, nawashauri wasomaji kuachana na njia hii ya kutafuta utajiri. Nawashauri wachague njia yoyote inayofaa na inawezekana kwa kufuatana na mazingira yanayomzunguka mtu husika. Mkulima au mfugaji anaweza kuzingatia fani hii na kutajirika sana. Kwa kweli hakuna mipaka, hasa hapa kwetu Tanzania kwa sababu ya wingi wa fursa za kuweza kujishughulisha na kuwa tajiri.
Maelezo ya kina juu ya aina ya biashara au mbinu unaweza kuzitumia kutafuta na kupata faida utayapata katika sehemu ya pili ya kitabu hiki.
Inawezekana kuwa tofauti kati ya mtu tajiri na mtu maskini inatokana na kile tulichojifunza kutoka kwa wazazi wetu. Wazazi maskini huwaambia watoto wao wajitahidi kusoma sana ili wapate maksi nzuri darasani na ili baadaye waweze kupata kazi nzuri. Wakati wazazi matajiri huwapa watoto wao elimu ya namna ya kutafuta fedha. Kwa kawaida tukiwa shuleni tunapewa ripoti ya masomo. Katika maisha tunatakiwa kuwa na ripoti yetu ya maisha nayo ni orodha ya mali tulizonazo ikiwa ni pamoja na elimu ya kuzaliwa na ya kusomea na fedha taslimu zile zilizo katika hifadhi mbalimbali.
Kwa kufuata tafsiri ya Umoja wa mataifa mtu masikini ni yule ambaye kipato chake hakizidi TShs 1,000 kwa siku.
Inawezekana kuwa mfumo wa kifedha wa mtu maskini ni mfumo ambao humfanya kutumia kipato chake chote kulipia matumizi huwa hana ziada wala uwezo wa kuweka akiba hana madeni na hana mali.
Mfumo wa fedha wa mtu mwenye kipato cha kati ni mfumo ambao humfanya kuwa na mali kama magari, nyumba na kadhalika. Mara nyingi mali hizo huwa zinapatikana kwa mikopo na hutumia mshahara kulipia matumizi na madeni, hasa kama madeni ni makubwa, mtu mwenye kipato cha kati anapaswa kumuona mshauri wa maswala ya biashara. Hatua anazoweza kuchukua ili kujikwamua na tatizo la madeni anaweza kulazimika kuuza baadhi ya mali zake ambazo amezinunua kwa kutaka kuonyesha ufahari tu na ambazo hazina umuhimu. Kwa mfano kama mtu ana magari matatu ya kutembelea, anaweza kuuza magari mawili kubaki na gari limoja na fedha atakayoiokoa kuiwekeza au kutumia kama mataji na kuanzisha biashara ili kujiongezea kipato.
Mfumo wa mtu tajiri ni mfumo ambao unamwezesha kuwa na biashara yake, kumiliki mali nyingi, kuwa na fedha nyingi katika akiba na awe ameziwekeza kwenye vitega uchumi vinavyolipa faida kubwa zaidi ya asiliamia kumi, kama vile nyumba za kupangisha na hisa. Mtu huyu hana wasiwasi na maisha. Anaweza kusafiri au kuugua lakini vitegauchumi vyake vinaendelea kumwingizia fedha. Siri kubwa ya matajiri ni uwezo wa kutumia fedha na kuziwekeza kupata faida kubwa.

Hiki ni kitabu cha vitendo. Yote unayoyasoma humu inabidi uyafanyie kazi ili
yakusaidie. Tofauti kati ya maskini na tajiri iko katika kuchukua hatua. Tajiri
hujifunza mambo ya kumwendeleza na kuchukua hatua kwa kutekeleza kwa vitendo
yale anayojifunza na anayoyaona yanaweza kumuinua kiuchumi. Maskini huwa anajifunza
mambo na kuyaacha kichwani bila kuchukua hatua au kuyafanyia kazi aliyojifunza
na hivyo fursa ya kupata utajiri inampita hivihivi. Kwa hiyo, kama unataka kuwa
tajiri anza mara moja kufanya yafuatayo:-
1. Anza kuweka akiba ya T.Shs 1,000 kila siku. Tengeneza kisanduku na
tumbukiza TShs. 1,000 kila siku. Zikifika TShs. 50,000 kafungue akaunti ya
TAJIRIKA, kwenye Benki ya “Standard Chatered”. Kisha endelea kuweka TShs.
30,000 kila mwezi. Jinsi mapato yako yatakavyokuwa yanaongezeka tenga asilimia
kumi (10%) ya mapato yako uweke akiba kila mwezi. Lengo lako liwe ni kuweka
TShs 10,000 au zaidi kila mwezi. Fedha unayoweka ni kama unapanda mbegu.
Kumbuka hii ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kwenye utajiri. Faida katika benki
hii ni kubwa. Inaanzia asilimia 6.5% kwa kianzio cha TShs. 50,000 hadi TShs.
5,000,000 na asilimia 10% kwa kiwango kinachozidi TShs. 10,000,000. Fedha
utakazoziweka huko usiziguse mpaka ukiona zimekuwa nyingi ndipo utaamua na
kupanga ukaziwekeze sehemu gani.
2. Jifunze pia mbinu za kutafuta fedha. Njia rahisi ni ya uhakika ya kukuwezesha kufanikiwa kiuchumi katika maisha ni kutafuta mshauri au mtaalamu anayejua mbinu za uongozi wa biashara ili akushauri vizuri juu ya yale unayonuia kutekeleza.
3. Inawezekana pia bado hujawa na biashara ya aina yoyote. Kama ndivyo anza kufanya utafiti kuona utafanya biashara gani. Mawazo ya biashara gani ufanye unaweza kuyapata katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. Kila mara hakikisha unatenga asilimia 10% ya mapato yako na kuweka kwenye akaunti yako ya TAJIRIKA. Kumbuka kwamba kuwa na biashara yako ni siri ya pili ya kuelekea kwenye kupata utajiri. Kama unayo biashara yako unaweza kumtafuta mtaalamu wa biashara kuangalia jinsi unavyoweza kuiboresha au kuipanua.
4. Panga malengo ya muda wa mwaka mmoja miaka mitano na miaka ishirini ili kuhakikisha kwamba unajikomboa kiuchumi. Malengo yako makuu yawe ni:- kuwa na akiba ya fedha za kutosha katika akaunti yako , kuwa na biashara yako, na vitega uchumi vya aina tofauti ambavyo unaweza kuvisimamia vizuri.
5. Kama wewe ni mwajiriwa, kipimo chako cha mafanikio kiwe ni kujiuliza swali, kama utaacha kazi yako ya mshahara utaweza kuishi kwa kutumia kipato chako cha pembeni kwenye biashara yako kwa muda gani? Mafanikio yako yatakuja pale utakapoweza kutumia kipato chako cha ziada bila kutegemea mshahara, na hapo ndipo unaweza kuacha kazi na kwenda kuimarisha biashara zako au kuendelea na kazi huku pia ukijiimarisha kibiashara.
6. Kama utafuata mpango wa namna hii na kujituma kwa juhudi na maarifa kwa muda wa miaka mitano (5) unaweza kuwa tajiri na maisha yako yanaweza kuwa mazuri.

0 comments:
Post a Comment