Utangulizi
Kila mtu mwenye mafanikio lazima
alianzia sehemu Fulani, na si rahisi mtu kupata mafanikio pasipo kupitia sehemu
Fulani. Ni lazima mtu awe na uhakika, uthubutu na moyo wa kufanya kile
anachokitazamia ni sehemu ya kufikia mafanikio yake. Zifuatavyo ni njia tano
ambazo mtu anaweza kupitia kufikia mafanikio
- Anza kidogo lakini fikiria vikubwa (start small, dream big)
Kuna ukweli
mmoja kuwa hakuna nguvu yoyote ya kuwaza/ kuota vitu vikubwa kama vidogo. Ili kuwa
mjasiriamali mwenye mafanikio ni lazima ujenge uwezo wa kuweza kufanyia kazi
ile sauti ndogo na kuifanya kuwa kubwa katika maono endelevu. Kwa kujenga huo
uwezo ndani yako utaweza kuona fursa ambazo watu wengine hawazioni. Vile vile kwa kuwaza/kuota
vikubwa ni rahisi kupata mafanikio kwa kile unachokusudia.
- Tambua vipaumbele vyako ( identify your priorities)
Ili kuwa
mjasiriamali mwenye mafanikio ni lazima uainishe vipaumbele vyako katika lile
wazo au mradi ambao unataka kutekeleza na kuwa na uthubutu katika kutekeleza. Hii
husaidia kuwa na misingi katika biashara uliyonayo/unayotaka kuanzisha na ni
vyema kuwa makini katika kutambua vipaumbele vyako.
- Pata hasara mara moja na usikubali tena kuapata hasara (fail fast & fail often)
Watu wazima
walisema kufanya kosa si kosa bali kurudia kosa ni kosa. Wajasiriamali wengi
wanashindwa kufikia malengo kwa sababu wengi wao wanaogopa kupata hasara lakini
ili kufikia kilele cha mafanikio ni lazima mtu akubali kufanya majaribio ya
kupata hasara ambayo yatamjengea uwezo
na ujasiri katika kukuza biashara yake.kwaiyo
mtu asiogope kufanya makosa. Ni lazima ujaribu kufanya makosa, ujifunze na
kujaribu tena. Na kama ukajaribu kufanya makosa na kukubali kushindwa huwezi
kuwa na mafakio yale unayotakiwa kuwa nayo.
- Tengeneza kikosi kizuri cha watu (create a solid team)
Kwa kuangalia
wale watu maarufu ambao tayari wamefikia katika kilele cha mafanikio unaweza
kuona walikuwa wamezungukwa na washauri wazuri ambao waliweza kuendeleza ndoto
zao na kuzifanya zenye mafanikio na za kweli. Ni muhimu kwa mjasiriamali
anayeanza akazungukwa na watu wenye tija katika kukuza na kuendeleza ndoto
iliyoko ndani yake katika kufikia kilele cha mafanikio ya ndoto yake.
- FOCUS
Kuwa mjasiriamali
ni rahisi sana kila mtu kuwa hivyo, lakini ukweli ni kwamba kupata faida
kunahitaji kuwa mtendaji mzuri wa kazi (Hard work), kujitoa (sacrifice) na
kujitambua (Determination) ili kuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio ni vyema
ukawa focused katika yale unayofanya. Na mtu aliyetambua ndoto yake waga
anaifanyia kazi mpaka ionjyeshe matunda.
MWISHO
kupitia hizo njia tano hapo juu nina imani kuwa zitaongeza uthamini wa ndoto yako na kukujengea ujasiri wa kuanza na kufikia mafanikio. Ni vyema kila mtu akaona ndoto yake ina uthamani hivyo anapaswa kuitunza na kuilea mpaka kilele cha mafanikio kwa kupitia hizi kanuni tano.
0 comments:
Post a Comment