KILIMO CHA VITUNGUU SWAUMU
-UTANGULIZI
Mahitaji ya hali ya hewa na udongo
Zao hili hupendelea hali ya hewa ya baridi na udongo tifu tifu na wenye rutuba. Sehemu nyingi zinazostawi vitunguu maji hufaa pia kwa zao hili. Maeneo ya mwinuko wa kiasi cha zaidi ya mita 1000 juu ya usawa wa bahari hufaa zaidi
- Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sen-timita 30 hadi 45
Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi mita 1.5 kutoka kati kati ya tuta na tuta na upana wa mita 1
- Maandalizi ya Mbegu
Kwanyua vipande/Vikonyo vya vitunguu sumu tayari kwa ajili ya kupanda katika nafasi. Mbegu sharti iwe imekaa kwa miezi mitano hadi sita tangu kuvuna ili iweze kuota. Ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri wa kitaalam ili kujua namna ya kutam-bua mbegu ya vitunguu saumu iliyo tayari kwa kupanda kwani ikipandwa kabla haijawa tayari haioti
- Upandikizaji
Tumia mashine—alama kuweka alama za kupandia katika nafasi ya sentimita 15 hadi sentimita 25 na mistari minne hadi sita kwa tuta
Hakikisha shamba lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda
- Palizi
Palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu
Magugu hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya viuagugu
- Mbolea
Tumia mbolea ya DAP wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji
- Matumizi ya viuatilifu
Matumizi ya viuatilifu yafanyike kila baada ya wiki mbili kwa ushauri wa wataalamu
Mavuno
Vitunguu saumu hukomaa miezi 6 tangu kupanda
0 comments:
Post a Comment