A.
MPASUKO WA
MVIRINGO
Hali hii
hutokea wkati mmea unapokosa maji ya kutosha, hasa wakati wa jua kali, ambapo
maji yaliyopo kwenye tunda hayalingani na maji yanayopotea angani (mvuke).
KUZUIA:
Ø
Mwagilia maji kama inavyotakiwa.
B. KUOZA
KITAKO
Kidonda cheusi
kilichodidimia huonekana kwenye kitako cha tunda. Kisha sehemu hii hunyauka na
ngozi huwa nyeusi. Hali hii hutokea zaidi wakati wa jua kali na katika sehemu
zenye udongo wenye chumvichumvi na tindikali nyingi. Pia nyanya nyingine huwa
na makunyanzi upanda wa chini wa tunda na kuoza. Sehemu hiyo huwa na rangi
nyeupe.
KUZUIA:
Ø Epuka kulima
kwenye maeneo yenye hali ya chumvichumvi na tindikali nyingi.
Ø Usibadilishe
nyakati za kumwagilia maji
C. MTUNDA
YA KIJANI KIBICHI
Sehemu ya juu
ya tunda huwa na rangi ya kijani kibichi kutokana na chanikiwiti kuwa nyingi.
Hali hii hutokea hasa wakati wa jua kali.
KUZUIA:
Ø Epuka kuweka
mbolea nyingi za chumvichumvi
Ø Punguza mwanga
wa jua kwa kufunika udongo na majani makavu.
D. MABAKAMABAKA
YA MATUNDA
Matunda yaliyopigwa na jua huwa namabakamabaka hasa
sehemu za ubavuni zilizopata jua kali.
KUZUIA:
Ø Epuka kupunguza matawi mengi kwa wakati mmoja hasa
katika sehemu zenye ukavu
0 comments:
Post a Comment