Utangulizi
Mkulima
anaweza kupunguza gharama, kuongeza rutuba kwenye udongo, mavuno pamoja na
kipato kwa kutengeneza mbolea mwenyewe.
Mimea
inaweza kukuonyesha inahitaji nini. Ni rahisi sana kugundua endapo mimea
haipati virutubisho vya kutosha. Majani kubadili rangi ni ishara tosha kuwa
mimea ina upungufu wa virutubisho. Ni lazima mkulima awe tayari kutatua tatizo
hilo kwa haraka kabla hali haijawa mbaya. Upungufu wa madini ya nitrojen na
fosiforasi ni jambo la kawaida kwa mimea. Virutubisho hivi vinahitajik kwa
kiasi kikubwa sana kwenye mimea hasa katika hatua ya ukuaji.
Hata
hivyo, ni muhimu kuelewa kwamba utatuzi unategemea hatua za kutunza udongo kwa
kipindi chote cha mwaka. Lisha udongo ili ulishe mazao yako; tumia mboji,
samadi, mbolea vunde, matandazo na utaratibu mzuri wa kupanda mazao kwa
mzunguko.
Kunyunyizia
kunafaa zaidi
Mkulima
anaweza kusaidia hatua hii ya kulisha mimea inayokuwa kwa njia ya kunyunyizia
mbolea ya maji. Kunyunyizia inasaidia kuipatia mimea virutubisho moja kwa moja
kupitia kwenye majani na shina.
Unaweza
kuona matokeo mazuri ya kuweka mbolea kwa kunyunyizia kulingana na kiwango cha
mavuno, uwezo wa mimea kukabiliana na wadudu pamoja na magonjwa, kuvumilia
ukame, na kuongeza ubora wa mazao. Mimea inakuwa na uwezo wa kunyonya mbolea
mara 20 zaidi ya unapotumia aina nyinginezo za uwekaji wa mbolea kwenye mimea.
Kutengeneza
mbolea ya maji
Aina
hii ya mbolea hutengenezwa kwa kuchukua kiroba kilichojazwa samadi, aina
mbalimbali ya mimea yenye virutubisho na inayoaminika kuwa dawa ya mimea.
Kiroba hicho kinafungwa kwenye kijiti, na kutumbukiza kwa kuning’inia kwenye
pipa lililojazwa maji. Kiroba hicho ni lazima kichukue kati ya kilo 30-50 za
samadi pamoja na aina nyingine za mimea kwa maji lita 200 (tazama mchoro).
Mkulima
anaweza kushika upande mmoja wa mti na kunyanyua na kushusha kila baada ya siku
tano ili kuchanganya na kuharakisha kutolewa kwa virutubisho zaidi. Kwa kawaida
mchanganyiko huo unakuwa na harufu kali sana maana Nitrojeni nyingi inayopatikana
hugeuka kuwa Amonia. Ni vizuri kufunika pipa ili kuzuia kuyeyuka kwa nitrojeni.
Harufu ikishaisha, ujue mbolea yako ipo tayari kwa matumizi. Ongeza maji na
utingishe vizuri kabla ya kutumia. Nyunyizia mimea yako kila wiki mpaka
utakapoona mabadiliko.
Tumia
mimea peke yake
Kama
unatengeneza mbolea ya maji kwa kutumia mimea peke yake, inashauriwa kutumia
aina nyingi za mimea kama vile mivule, mibangi mwitu, majani ya minyanya,
mwarobaini, mashona nguo, pamoja na vitunguu saumu. Aina hii ya mimea inasaidia
sana katika kuzuia magonjwa, wadudu na kutoa virutubisho muhimu kwa mimea
vinavyosaidia mkulima kupata mazao bora bila gharama ya ziada ya kununua
virutubisho.
Vigezo
vya kunyunyizia
Ili
mbolea ya kunyunyizia iwe na matokeo mazuri, vigezo vifuatavyo vifuatwe:
• Inashauriwa kutumia mbolea iliyochanganywa vizuri ili kuepukana na kuunguza mimea.
• Acha maji utakayotumia kuchanganyia mbolea yako nje katika pipa lililowazi usiku kucha, hii inasaidia kutoa madini hatarishi, na kufanya mchanganyiko wenye faida kwa mimea.
• Tingisha vizuri. Chembechembe ndogo ambazo hazikuyeyuka zinaweza kuziba mdomo wa bomba la kunyunyizia.
• Matokeo mazuri yanaweza kupatikana endapo mbolea imechanganywa vizuri na kunyunyiziwa wakati hakuna upepo.
• Nyunyiza mbolea wakati wa asubuhi au jioni wakati hakuna joto na upepo ukiwa umepungua.
• Inashauriwa kutumia mbolea iliyochanganywa vizuri ili kuepukana na kuunguza mimea.
• Acha maji utakayotumia kuchanganyia mbolea yako nje katika pipa lililowazi usiku kucha, hii inasaidia kutoa madini hatarishi, na kufanya mchanganyiko wenye faida kwa mimea.
• Tingisha vizuri. Chembechembe ndogo ambazo hazikuyeyuka zinaweza kuziba mdomo wa bomba la kunyunyizia.
• Matokeo mazuri yanaweza kupatikana endapo mbolea imechanganywa vizuri na kunyunyiziwa wakati hakuna upepo.
• Nyunyiza mbolea wakati wa asubuhi au jioni wakati hakuna joto na upepo ukiwa umepungua.
0 comments:
Post a Comment