FAIDA ZA TANGO KIAFYA KATIKA MWILI WA MWANADAMU


1.    Tango ni chanzo kizuri cha vitamin hasa vitamin B.

2.    Tango husaidia kuondoa sumu mwilini. Asilimia 95 ya tango ni maji hivyo huupa mwili maji na kuusaidia kuondoa sumu mwilini kwani pia lina vitamin karibu zote ambazo mwili huhitaji kila siku.

3.    Tango pia hutumika kwenye matunzo ya ngozi/urembo ambapo huwekwa machoni na kuondoa uvimbe hasa kwa watu ambao umri umeanza kusogea kwani tango lina virutubisho vya kuondoa uvimbe  wa namna hiyo na pia lina silicon na sulfur ambazo husaidia kwenye ukuaji wa nywele.

4.    Tango lina virutubisho kama lariciresinol, pinoresinol na secoisalariciresinol ambavyo kulingana na tafiti mbali mbali za magonjwa ya kansa husaidia kupunguza aina mbali mbali za kansa kama kansa ya matiti, kansa ya mifuko ya mayai kwa wanawake, kansa ya kizazi kwa wanawake na kansa ya tezi dume kwa wanaume.

5.    Tango husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani.

6.    Tango huondoa hangover kwa watumiaji wa pombe kwani lina vitamin B ambazo husaidia kupunguza ukali wa maumivu ya kichwa pale unapoamka asubuhi ila unatakiwa kula kabla ya kulala ili uamke ukiwa vizuri.

7.    Tango husaidia kupungua uzito na mmeng’enyo uende vizuri. Kutokana na kiasi kidogo cha sukari kilichopo kwenye tango na kiasi kikubwa cha maji, tango ni tunda sahihi kukusaidia upungue uzito. Kiasi cha maji kilichopo kwenye tango na Kamba Kamba zake huusaidia mwili kuondoa sumu katika mfumo wa chakula na kusaidia mmeng’enyo wa chakula. Unapokula tango kila siku pia hukusaidia wewe mwenye choo kigumu au usiyepata choo kabisa kwa muda mrefu kuondokana na tatizo hilo.

8.    Tango husaidia wagonjwa wa kisukari, hupunguza mafuta mafuta kwenye mishipa ya damu na huweza kudhibiti shinikizo la damu aina zote mbili (Low and high blood pressure). Tango lina hormone ambayo huhitajika kwenye chembechembe za kongosho (pancreatic cells) ilikuweza kutengeneza insulin ambayo husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye mwili hivyo kuwasaidia wagonjwa wa kisukari. Pia watafiti wamegundua kuwa kuna kirutubisho kiitwacho sterol kwenye tango ambacho husaidia kupunguza mafuta kwenye mishipa ya damu. Tango lina kiwango kikubwa cha potassium, magnesium na Kamba Kamba ambazo husaidia sana kudhibiti shinikizo la damu aina zote yani high blood pressure na low blood pressure.

9.    Husaidia afya ya viungo, huondoa gout na ugonjwa wa baridi yabisi (Arthritis). Tango ni chanzo kizuri cha silica ambayo inafahamika kusaidia afya ya viungo kwa kuimarisha viunganishi vya viungo (connective tissue). Pia tango lina Vitamin A, B1, B6, C & D, Folate, Calcium, Magnesium na potassium ambavyo hufanya tango linapochanganywa na juice ya karoti huweza kutibu gout na baridi ya yabisi (arthritis) kwa kupunguza kiwango cha tindikali kwenye mkoo (Uric acid).

10.    Kutokana na maji na virutubisho vilivyopo kwenye tango, tunda hili husaidia kupunguza homa pale inapopanda.
Share on Google Plus

About kilimo uchumi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment