FAIDA ZA KUTUMIA PILIPILI


Kwa uchache ningependa kuongelea faida ya pilipili katika mwili wa mwanadamu maana ziko nyingi kulingana na watafiti mbalimbali. Nitaendelea kuonyesha faida mbalimbali za matumizi mbalimbali ya mazao yatokanayo na kilimo na baadaye tutaweza kuona namna ya kuzalisha katika eneo dogo hasa wale wa mjini kwa manufaa ya afya.

1. Pilipili inasaidia sana kusawazisha sukari kwenye damu

2. Ulaji wa pilipili kunaweza kunawasaidia sana watu wanene (overweight) au wanao ugua ugonjwa wa kisukari.

3. Utafiti unaonyesha kwamba ukila Pilipili kunaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kudhibiti na kusawazisha insulini kwa 60%. baada ya kula chakula.

4. Pilipili husaidia kupunguza maumizi na uvimbe kwenye tezi na vilevile huwasaidia wagonjwa wa rheumatoid na arthritis kupata nafuu. Vile vile husaidia kuondoa mkusanyiko wa damu sehemu moja ya mwili

5. Pilipili usaidia kufungua kwa haraka na kwa ufanisi pua zilizoziba kwa mafua, kuruhusu kupumua kwa urahisi zaidi.

6. Pilipili pia husaidia kupunguza upatikanaji wa saratani ya kwenye tumbo (Stomach Cancer)

7. Pilipili usaidia kuongezeka kwa kiwango cha metabolic, ambayo husaidia kuchoma mafuta, ulaji wa pilipili kunaweza kuinua kiwango na metabolic yako hadi 23% ndani ya masaa 3.

8. Kula pilipili usaidia kupunguza cholesterol, na kupunguza kiasi cha fibrin katika damu

ANGALIZO: Kula pilipili kupita kiasi ni hatari pia kwa afya yako
Share on Google Plus

About kilimo uchumi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment