shambani ili wakati wa kung’oa miche, mizizi ishikamane vizuri
na udongo.
• Mashimo yaandaliwe mapema katika nafasi zinazopendekezwa.
• Miche mizuri ni ile iliyo na afya nzuri, yenye majani kati ya 3 - 5, na iliyo na mizizi yenye afya na ya kutosha.
• Miche ioteshwe siku hiyo hiyo ya kung’oa toka kitaluni.
• Hamishia miche shambani wakati wa jioni ili kuepuka mionzi mikali ya jua. Vipindi vya baridi kama kuna ulazima wa kufanya hivyo; miche inaweza pia kuhamishiwa shambani asubuhi.
• Ng’oa miche kwa uangalifu pamoja na udongo wake kwa kutumia vifaa husika ili mizizi isidhurike.
• Chagua miche yenye afya tu.
• Panda miche shambani kimo kile kile ilichokuwa kitaluni.
• Mwagilia miche maji ya kutosha mara baada ya kupanda.
0 comments:
Post a Comment