MNYORORO WA THAMANI WA ZAO LA ALIZETI


kutoka Kushoto ni Rose Simion kutoka Ulemo na Grace ernest kutoka Shelui
Leo katika kutembelea maonyesho ya wakulima nane nane yanayofanyika kikanda  kwa kanda ya kati yanafanyika Dodoma na Kitaifa yanafanyika Mkoani Lindi, nilifanikiwa kukutana na wakinamama wawili mmoja anaitwa Grace ernest kutoka Shelui na Rose Simion kutoka Ulemo wakiwa ni wawakilishi kutoka kwenye vikundi vyao, katika mojawapo ya banda la Wilaya ya iramba wakiwa na bidhaa zitokanazo na mafuta ya alizeti yaliyoongezewa thamani. Katika mnyoro wa thamani wa zao la alieti wamefanikiwa kutengeneza mafuta ya kupaka (mgando), dawa ya mbu (mosquitoe reppelant), Dawa ya ngozi (medicinal oil), Rangi ya viatu pamoja na mkaa utokanao na mabaki ya zao la alizeti.
rose mafuta ya dawa
wanasema wamepata mafunzo hayo kupitia mradi wa PEML (Producer empowerment and Market linkage) kupitia MIVARF wakiwa chini ya usimamizi wa RCCL (Rural Consultancy company Limited) bofya hapa wakiwa  watoa huduma (Service Provider) katika eneo lao la mradi. Pia kupitia mtoa Huduma RCCl wamefanikiwa kuunganishwa na masoko ya bidhaa zao, elimu juu ya uzalishaji wa zao la alizeti wenye tija, elimu ya fedha, usindikaji nk.

Malaika mafuta ya kupaka
Rose simion akiwa na mafuta ya Alizeti



Share on Google Plus

About kilimo uchumi

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Post a Comment